Lionel Messi atoa sababu ya kushindwa kuwa na urafiki mzuri na Cristiano Ronaldo

Staa wa soka wa klabu ya Barcelona Lionel Messi ametoa sababu inayofanya asiwe na urafiki mzuri na Cristiano Ronaldo.
Akihojiwa na Marca, Messi anasema “Siwezi kuwa Best Friend wa Cristiano Ronaldo sababu hatupati muda mwingi wa kukaa pamoja na kujuana zaidi na kujenga urafiki”

Messi kupitia Barcelona na Ronaldo kupitia Real Madrid wote ni mastaa wakubwa wa soka katika ligi ya La Liga na dunia nzima, wameshinda tuzo kubwa kama Ballon d’Or awards (Messi 5, Ronaldo 4) huku Ronaldo akitajwa kama mchezaji anayetegemewa kushinda ya mwaka 2017.

No comments