Vanessa na Jux mambo moto moto

 Kwenye FIESTA ya Dar es salaam Mastaa wa Bongofleva Jux na Vanessa Mdee walifanya yao kwenye stage ambapo V Money alilainika na kumsamehe Jux ili warudiane baada ya Jux kuwatanguliza kaka zake Q Chief na Cassim wamuombee msamaha.
Baada ya kushuka kwenye stage Vanessa alihojiwa na AyoTV na kuulizwa umemsamehe? >>> “ Yani sio kwa yale ma-melody ya Cassim na Q Chief utaacha kusamehe? lakini tutaona… tutafanyia kazi, Jux alijiandaa sana na anajua k
wamba mimi ni Shabiki Mkubwa wa Q Chief na Cassim”
“ Najua amefukua yale maongezi ya zamani ambayo tulikuwa nayo kuhusiana na muziki na vitu ambavyo naenda, ametumia jinsi gani anavyonifahamu ” – Vanessa

No comments